1574627560
Afrika Ya Mashariki

Advertise on podcast: Afrika Ya Mashariki

Categories
Country
United States
This podcast has
24 episodes
Language
English
Publisher
RFI Kiswahili
Explicit
No
Date created
2021/07/01
Latest episode
2026/09/26
Average duration
10 min.
Release period
41 days

Description

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.

Unlock Afrika Ya Mashariki podcast Email contact info,
Listeners & Audience details

Email contact information

Direct podcast contact details

Listeners

Audience numbers & engagement insights

Audience details

Podcast Insights

Podcast episodes

Check latest episodes from Afrika Ya Mashariki podcast


Safari ya Sudan Kusini kuelekea uchaguzi wake mkuu wa kwanza
2026/09/26
Baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 15 tangu kupata uhuru mwaka 2011, Sudan Kusini imepanga kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa kitaifa tarehe 22 Desemba 2026.  Je, uchaguzi huo utafungua ukurasa mpya wa demokrasia au utaibua mzozo mwingine wa kisiasa katika taifa hilo changa zaidi barani Afrika?
EAC: Kesi za kisiasa au utawala wa kisheria
2026/09/11
Katika kipindi cha miaka ya karibuni, viongozi wa upinzani katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wameendelea kujikuta mahakamani wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo uhaini.  katika Makala ya Afrika Mashariki, tunaangazia mwenendo wa kesi zinazowakabili viongozi wa upinzani katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, je, ni ishara ya kuimarika kwa utawala wa sheria au kuna maswali yanayoendelea kuulizwa kuhusu ushindani wa kisiasa?
Kenya yaanza safari ya kutafuta dira mpya, ruwaza ya 2030 ikielekea kufika ukomo
2026/08/21
Kenya imeanza safari ya kutafuta dira mpya ya maendeleo baada ya Ruwaza ya Taifa ya Maendeleo 2030 kuelekea kufikia ukomo wake. Safari hii inakuja wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ikiwa na dira yake ya pamoja ya mwaka 2050, inayolenga kujenga ukanda wenye uchumi shindani, miundombinu iliyounganishwa, viwanda, biashara, ajira na maendeleo ya watu.
Tanzania: Nanenane imebaki maonesho ya kilimo au imegeuka soko la biashara?
2026/08/12
Tunaangazia mjadala kuhusu mustakabali wa maonesho ya nanenane nchini Tanzania. Je yaendelee kuwa jukwaa la teknolojia za kilimo pekee au yafungue milango kwa biashara zote?
Safari ya Tohara ya kitabibu kutoka mila hadi afya ya umma
2026/08/01
Katika Makala ya wiki hii, tunaangazia safari ya Tohara ya kitabibu kutoka mila hadi afya ya umma.
Mazungumzo ya kitaifa yanaweza kuponya majeraha ya DRC?
2026/07/24
Katika Makala ya Afrika Mashariki, tunaangazia mchakato wa mazungumzo ya kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nafasi ya viongozi wa dini na matarajio ya wadau wa kisiasa katika kutafuta amani na maridhiano ya kudumu.
CCM na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano.
2026/07/15
Baada ya mvutano wa kisiasa uliojitokeza mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita huko Zanzibar, sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano. Lakini je, makubaliano hayo yatafungua ukurasa mpya wa demokrasia, au ni hatua ya kujenga utulivu kuelekea uchaguzi ujao? Makubaliano hayo yaliyosainiwa Julai 9, 2026 yanajumuisha mapitio ya Katiba, mageuzi ya uchaguzi, maboresho ya mfumo wa sheria, kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma, kuundwa kwa chombo cha kisheria cha kusimamia utekelezaji wa makubaliano pamoja na kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hafla ya utiaji saini imefanyika Ikulu Zanzibar mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na viongozi wa dini, serikali na wadau mbalimbali. Karibu katika Makala ya Afrika Mashariki hii leo tunaangazia makubaliano ya kisiasa kati ya CCM na ACT-Wazalendo Zanzibar, matarajio yake, changamoto zake na athari zake kwa mustakabali wa demokrasia visiwani  karibu tuwe pamoja hadi tamati.
Hali ya Ziwa Victoria na changamoto zinazolikabili
2026/05/30
Tunaangazia hali ya Ziwa Victoria, changamoto zinazolikabili pamoja na juhudi za kikanda zinazofanyika kulinusuru ziwa hilo ambalo ni mhimili wa uchumi na maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki. Ziwa Victoria, ambalo ni tegemeo la mamilioni ya wananchi wa Afrika Mashariki, linaendelea kukumbwa na changamoto kubwa za mazingira, uvuvi haramu na uchafuzi wa maji. Ripoti mpya ya mwaka 2025 imeonya kuwa bila hatua za haraka, uchumi, afya na maisha ya wananchi wa ukanda huo yako hatarini. Jumuiya ya Afrika Mashariki imezindua ripoti ya mwaka 2025 kuhusu hali ya Bonde la Ziwa Victoria, ikieleza changamoto zinazoendelea kulikabili ziwa hilo ikiwemo uvuvi haramu, uchafuzi wa mazingira na kupungua kwa samaki muhimu wa biashara. Ripoti hiyo yenye sura tisa imechambua kwa kina hali ya ikolojia, mazingira, viwanda, mipango miji, ajira, utalii pamoja na maendeleo ya miundombinu katika ukanda wa Ziwa Victoria.
Tanzania: Ripoti ya Tume ya uchunguzi kuhusu vurugu za uchaguzi mkuu wa Oktoba
2026/05/02
Makala ya Afrika Mashariki, ikiangazia juu ya ripoti ya Tume ya uchunguzi wa matukio ya wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa October 29, 2025 nchini Tanzania.
Kumbukizi ya miaka 32 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994
2026/04/11
April 7, 1994 ni siku ya ambayo historia ya Rwanda ilianadikwa kwa wino mwekundu kumaanisha hatari, kifo cha Rais zamani wa Taifa hilo Juvenal Habyarimana aliuawa akitokea nchini Tanzania katika mchakato wa kusaka amani nchini Rwanda, baada ya waasi wa kundi la RPF wakati huo, ambalo kwa sasa ni chama kilichopo madarakani, kuanzisha vita dhidi ya serikali ya Juvenal Habyarimana, wakimtuhumu kuwatenga raia wa Rwanda kutoka jamii ya watutsi.   Hapo ndipo ghasia zikazuka kote nchini humo kwa jamii ya Wahutu na Watutsi kushambuliana vikali kutoka mijini hadi katika vijiji.
Kasi na mapokeo ya ueneaji wa akili mnemba barani Afrika
2025/04/11
Karibu katika ya Afrika mashariki hii leo macho na masikio ya Makala haya yanatazama kasi na mapokeo ya ueneaji wa akili mnemba barani Afrika tukienega katika Mkutano wa Kimataifa wa AI kuhusu Afrika 2025, unaofanyika Kigali nchini Rwanda Mwandalizi na  msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe soote hadi tamati
Je una ufahamu juu ya ulinzi wa taarifa binafsi ?
2025/04/05
Kasi ya ugunduzi na uvumbuzi katika maswala ya sayansi na teknolojia na ujio wa Internet sanjali na matumzi ya mitandao ya kijamii yanafanya wajamii kuwa katika hatari kumbwa kupoteza usiri wa taarifa zao.  Baada ya mabadiliko makubwa ya teknolojia yamesababisha taarifa za watu kuwa ni moja ya mtaji mkubwa kwa watu wengine na makampuni makubwa  Tanzania kama yalivyo mataifa mengine ya Afrika mashariki imekutunga sheria rasmi ya kulinda haki kulindiwa taarifa binafsi Lakini sio kulinda tu taarifa binafsi lakini pia kuhakikisha taarifa hizo zinamfaidisha moja Kwa moja mlengwa wa taarifa endapo zinatakiwa kutumiwa Kwa matumizi fulani.  Msikilizaji wa RFI Kiswahili karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama kuangaza na kumulika kwa namna gani wakazi wa Afrika mashariki wanauelewa juu ya ulinzi wa taarifa binafsi sanjali na juhudi za mataifa katika kulinda maswala hayo Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe hadi tamati
Tatizo la kifua kikuu (TB) katika mataifa ya Afrika Mashariki
2025/03/29
Maambukizi ya kifua kikuu yanaweza kuenezwa kwa urahisi katika miji mikubwa na maeneo ya umma ambapo kuna mkusanyiko mkubwa wa watu, kama vile vituo vya mabasi, masoko, na hata sehemu za kazi kama waendesha bodaboda wanavyojihusisha.     Msikilizaji wa RFI Kiswahili karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwana kuangaza namna waendesha bodaboda wanaweza kuchukua tahadhari ya kupambana na maambukizi ya kifua kikuu Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati.
Tanzania: Namna wakaazi wa vijijini wanafikiwa na huduma za maji
2025/03/15
Namna wakazi wa maeneo ya vijijini wanafikiwa na huduma za maji nchini Tanzania.
Athari za mgogoro wa DRC katika mataifa ya Afrika
2025/03/08
Mgogoro wa Mashariki ya DRC umeendelea kwa miongo kadhaa, na bado ni moja ya changamoto kubwa za kiusalama na kisiasa Barani Afrika. Katika Mashariki ya DRC, kuna makundi ya waasi kama vile M23, ADF, Twirwaneho, ambayo yameongeza umwagaji damu na kusababisha maelfu ya watu kuhama kutoka maeneo yao. Siasa za kikanda, ushindani wa madaraka kati ya mataifa kama Rwanda yana iweka DRC njia panda kila uchao   Karibu katika Makala ya Afrika mashariki  hii tunangaza mgogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu, hasa katika majimbo ya mashariki ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tanganyika, kutokana na migogoro ya silaha na mapigano baina ya jamii. Mnamo Septemba 2024, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)

Podcast reviews

Read Afrika Ya Mashariki podcast reviews


0 out of 5
0 reviews

Podcast sponsorship advertising

Start advertising on Afrika Ya Mashariki relevant audience podcasts


What do you want to promote?