Advertise on podcast: Siha Njema
Categories
This podcast has
24 episodes
Publisher
RFI KiswahiliExplicit
No
Date created
2021/07/01
Latest episode
2026/10/13
Average duration
10 min.
Release period
8 days
Description
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Podcast episodes
Check latest episodes from Siha Njema podcast
Kwa nini afya ya akili ni swala muhimu kwa wagonjwa wanaougua magonjwa sugu
2026/10/13
Shirika la afya duniani ,WHO limesema watu zaidi ya milioni 150 barani Afrika wana hitaji huduma za afya ya akili.
Kutokana na idadi hii inayopanda kila wakati ,watalaam wa afya wanasisitiza wagonjwa walio kwenye matibabu ya magonjwa yasiyoambukizwa sharti kufuatiliwa pia kwa matatizo ya afya ya akili ,chini ya mpango wa huduma za afya jumuishi.
Wataalam wanasema matibabu ,gharama kubwa na mabadiliko ya haraka yanayoambatana na magonjwa haya yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha matatizo ya afya ya akili kwa mgonjwa
Dawa zinazotumika pia zinaweza kuwa chanzo cha matatizo kama msongo wa mawazo,sonona na kiwewe miongoni mwa wagonjwa hao.
Kifafa cha mimba bado kinasababisha vifo vingi vya akina mama na watoto Afrika
2026/10/07
Kifafa cha mimba hali inayohusishwa na shinikizo kubwa la damu mama anapokuwa mja mzito kuanzia wiki 20 za mimba na inaweza kujitokeza pia pindi mama anapojifungua ,ni hali ya dharura na tishio kubwa kwa akina mama waja wazito
Watalaam wanahoji kuwa hatari yake hutokana na kwamba dalili zake wakati mwingi hufanana na dalili za kawaida za mama mja mzito
Ni kutokana na hili mashirika ya kijamii kutoka mataifa matano ya Afrika yanashinikiza uwekezaji kwenye kubainisha ,kuzuia na kutoa huduma kwa akina mama waja wazito.
Isitoshe ushirika kwa wanaume kwenye maswala ya uzazi ili wanapokuwa wana ufahamu wanaweza kusaidia kwenye mapambano hayo
Wagonjwa wa saratani wanavyochanganya matibabu ya hospitali na mazoezi
2026/10/01
Wagonjwa wengi wa saratani mara nyingi huhisi kulemewa na madhara yanayotokana na matibabu makali ambayo wanabidi kutumia kwa muda mrefu.
Kurahisisha safari hiyo kituo cha Faraja Cancer Support Trust eneo la Parklands Nairobi kimewapa fursa ya kufanya mazoezi ; na kucheza muziki huku wakiendelea na matibabu hayo.
Wengi ambao wamekuwa wakishiriki mazoezi hayo wanasema miili yao ina uimara zaidi, wana ari mpya kupambana na wanaongeza furaha katika maisha yao kutokana na kupata marafiki ambao wanahimizana namna ya kuushinda ugonjwa wa Saratani.
Mchakato wa kupatikana chanjo mpya dhidi ya TB kufikia mwaka 2029
2026/09/22
Chanjo mpya za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB zitakuwa tayari kufikia mwaka 2029
Hadi sasa chanjo 16 zimekuwa zikifanyiwa majaribio na ikiwa zitaidhinishwa zitaokoa maisha ya watu zaidi ya milioni saba kufikia 2050 haswa katika mataifa yanayoendelea.
Kwa miongo kadhaa chanjo ya pekee ambayo imekuwa ikitumika kuzuia TB ni chanjo ya BCG ambayo mtoto anapewa pindi anapozaliwa.
Wanaharakati wanakiri hatua muhimu zimepigwa kupambana na TB ila uwepo wa chanjo itakuwa hatua muhimu katika mapambano hayo.
Kwa nini kilimo sharti kuzingatiwa kumaliza njaa barani Afrika
2026/09/19
Ripoti ya mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa yameonesha Afrika bado ina watu wengi ambao wanakabiliwa na njaa. Hii ni licha ya Afrika kuwa sehemu inayofanya kilimo .
Watalaam wanasema kilimo kimeathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi kama vile mafuriko,ukame na sasa hivi vijana wengi hawapendi kilimo
Hivi basi nini kifanyike kuhakikisha kuwa kuna lishe bora barani Afrika? Dkt Calistus Kundu mkurugenzi wa mamlaka ya kilimo na chakula nchini Kenya anafafanua.
Kisukari inaendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wa macho nchini Kenya
2026/09/09
Magonjwa yanoyohitaji matibabu ya muda mrefu ukiwemo kisukari unaendelea kusababisha watu wengi kupata matatizo ya macho au kupoteza uwezo wa kuona
Afrika kukabiliana na usugu wa vimelea vifo vikitarajiwa kuvuka milioni 4
2026/09/02
Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika ,Africa CDC kimeonya vifo vinavyohusishwa na usugu wa vimelea vinatarajiwa kuvuka milioni 4 mwaka wa 2050
Mashirika ya kikanda yanasisitiza utekelezwaji wa pamoja wa mikakati ya kukabiliana na usugu wa vimelea ikiwemo afya ya mifugo ,matumizi mazuri ya dawa za antibiotics na dawa za kunyunyuzia mimea kwenye sekta ya kilimo.
Watalaam wa afya wanaonya dawa hadi asilimia 70 zinatumika kwa wanyama na nyingi yazo huishia kwenye vyakula kama nyama,maziwa na hatimaye kusababisha usugu wa vimelea kwenye dawa zinazotumika kwa matibabu ya wanadaam
Mapambano dhidi ya Ebola Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
2026/08/28
Ebola imekamilisha siku 100 tangu ilipotangazwa na bado bado haijadhibitiwa
Shirika la kimataifa la VillageReach miongoni mwa mashirika yaliyoalikwa na utawala wa Kinshasa kusaidia juhudi za kudhibiti mwambao hatari wa Ebola Bundibugyo linazungumzia kuhusu mapambano hayo.
Baadhi ya changamoto zinazofanya ugumu mapambano hayo ni ukosefu wa uaminifu kati ya wananchi na serikali ,tamaduni na pia taarifa za uongo.
Kwa nini bima ya afya ya msafiri ni sharti muhimu kwa mataifa ya Afrika
2026/08/18
Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko
Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.
Unaweza kuendelea kunyonyesha hata baada ya kutenganishwa kwa muda na mwanao
2026/08/11
Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi.
Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.
Kwa nini watalaam wanahoji maumivu makali wakati wa hedhi si kawaida
2026/07/31
Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida
Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.
Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa
2026/07/21
Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu
Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.
Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya
2026/07/21
Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka kutokana na sumu ya nyoka.Katika makala haya ya siha njema tunaangazia kijiji cha Kapua kwenye kaunti hiyo .
Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma
2026/07/10
Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi
Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea
Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya
2026/06/30
Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi ya kila mara.
Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya madini ambavyo vyakula au vinywaji vinavyouzwa vinafaa kukidhii au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,sasa ipo mbioni kuja na sheria kushinikiza maandishi ya kuonya kuhusu vyakula venye mafuta ,sukari na chumvi nyingi kupachikwa kwenye bidhaa za vyakula na vinywaji