1578277330
Vijana na Mapenzi

Advertise on podcast: Vijana na Mapenzi

This podcast has
36 episodes
Language
English
Explicit
No
Date created
2021/07/26
Latest episode
2022/06/16
Average duration
11 min.
Release period
20 days

Description

Ni jukwaa la kila wiki la kuzungumzia mapenzi miongoni mwa vijana; mahusiano, kuchumbiana na mengi yaliyowakaa mioyoni.

Unlock Vijana na Mapenzi podcast Email contact info,
Listeners & Audience details

Email contact information

Direct podcast contact details

Listeners

Audience numbers & engagement insights

Audience details

Podcast Insights

Podcast episodes

Check latest episodes from Vijana na Mapenzi podcast


Vijana na Mapenzi Podcast; Je, vijana hutumia mbinu zipi kukatiana?
2022/06/16
Washauri wa masuala ya mapenzi watakweleza kwamba huwa ni kibarua kumtafuta mchumba na hasa mtu mtakayefaana maishani. Ili kumpata mpenzi ni lazima kwanza umtafute. Lakini je, ni mbinu zipi ambazo hutumiwa katika kutongoza? Msichana naye anaweza kufanya nini ili kumvutia mwanamume ambaye anampenda bila kutoa taswira kwamba ndiye anayemfukuzia mwanamume? Vijana na washauri wanatoa kauli zao kuihusu mada hii.
Vijana na Mapenzi Podcast: Je, wanaume ni watu wa kuaminika kuhusu upangaji uzazi?
2022/05/26
Katika siku za hivi karibuni yamekuwapo majaribio ya dawa za upangaji uzazi ambazo pia zinaweza kutumika miongoni mwa wanaume. Iwapo dawa hizo zitaanza kutumika, je, wanaume wanaweza kuaminika katika kuzimeza dawa hizo ama utakuwa mchezo wa paka na panya kati yao na wake zao? Tumezungumza na wananchi vilevile mshauri kulihusu suala hili.
Vijana na Mapenzi; inakera kwa mume kushauriwa na wazaziwe kabla ya kufanya lolote?
2022/05/05
Mwanamume anapokuwa mtu mzima, wengi hutarajia kwamba awe mwenye kujitegemea kimawazo na hata kuweza kujifanyia maamuzi ya busara. Hata hivyo, kuna wanaume ambao huitwa 'mamas boy' ambao hushtumiwa kwa kutojitegemea kimawazo na kuwasikiliza zaidi wazazi kabla ya kufanya maamuzi muhimu. Je, ni sawa kwa mume kuzingatia zaidi ushauri wa mzazi badala ya mkewe?
Vijana na Mapenzi Podcast; Mwanamke mwenye mtoto, atapataje mume mwaminifu?
2022/04/21
Mwanamke anapopata mtoto nje ya ndoa ama kumzaa mtoto katika ndoa kisha kutengana na mumewe, wapo wanaojipata katika njia panda anapotafuta mchumba. Baadhi huhofia kuwa katika mapenzi kwa hofu ya kulaghaiwa tena na hofu ya kupata mwanamume atakayempenda pamoja na mwanawe. Je, mwanamke huyu afanye nini ili ampate mchumba wa kumwamini?Tunaliangazia suala hili kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile mshauri.
Vijana na Mapenzi: Utajuaje mpenzi wako ana mahusiano mengine?
2022/04/07
Description. Wapenzi wanapokuwa katika mahusiano, mara nyingine huibuka hali za kutokuwa waaminifu. Katika kipindi hiki tuaangazia namna ya kumtambua mtu ambaye si mwaminifu kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile mshauri.
Vijana na Mapenzi Podcast: Je, ni sawa kwa wapenzi kuandamana kila mahali, mfano shopping, saloon, kinyozi?
2022/02/24
Wapenzi huoneshana upendo wao kwa njia mbalimbali mfano kushikana mikono katika maeneo ya umma, kupigana pambaja na wengine kupigana mabusu hadharani. Lakini je, ni sawa kwa wapenzi kuandamana mara kwa mara mfano kwenye saloon, kinyozi na kadhalika ama hali hiyo huenda ikachangia kuzoeana sana kiasi cha kusambaratisha uhusiano? Tumewashirikisha wananchi kulihusu suala hili vilevile kupata kauli ya mshauri.
Vijana na Mapenzi Podcast: Ni lazima mpenzi wako akupe zawadi siku ya Valentines?
2022/02/10
Ni msimu mwingine wa sherehe ya siku ya wapendanao tarehe 14 Februari. Siku hiyo hutumiwa na wapenzi wengi kuoneshana upendo. Baadhi hununuliana zawadi na hata kujitengea muda wa kufurahia mapenzi yao. Hata hivyo kwa wengine ni siku ya kawaida tu. Tunaangazia umuhimu wa siku hii na iwapo kuna ulazima wa kumpa zawadi umpendaye.
Vijana na Mapenzi Podcast: Kuwasiliana na mpenzi mliyetengana ni sawa?
2022/01/27
Mtu anapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi, mara nyingine hujipata katika hali ambapo analazimika kutengana na mpenzi wake. Kuna wale ambao husitisha kabisa mawasiliano kati yao huku wengine wakiyaendeleza licha ya kutengana. Je, ni sawa kuwasiliana na uliyetengana naye? Wananchi wanatoa kauli zao wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga. Aidha, washauri wawili, Rachel Mahungu na Malkia wa Vijembe wanatupambia podcast hii kwa ushauri nasaha.
Vijana na Mapenzi Podcast: Urafiki wa mwanamke na mwanamume bila mapenzi, inawezekana?
2022/01/14
Katika jamii, uhuru wa kutangamana huwafanya watu kuwa na marafiki, washirika wa kibiashara, kisiasa na kadhalika. Lakini je, inawezekana kwa mwanamume na mwanamke kuwa marafiki tu bila kuhusika kimapenzi, kwa kimombo inaitwa platonic friendship. Wananchi wanatoa kauli zao kulihusu suala hili. Vilevile tuna hoja za mshauri.
Vijana na Mapenzi Podcast: Sihamii kwa mume; soko ni mbali- maisha magumu
2021/12/09
Awamu hii ya Vijana na Mapenzi inaangazia kisa cha mwanadada ambaye licha ya kuolewa, hataki kwenda kuishi na mumewe na kupendelea aishi tu alikozoea kabla ya kuolewa. Anasema kwamba anakoishi, maisha ni rahisi kulinganisha na kwa mumewe. Tunaliangazia suala hili kwa kushirikisha kauli za wananchi na wataalam.
Vijana na Mapenzi Podcast: Waweza kumwacha mpenzi mwenye pesa kwa sababu gani?
2021/11/26
Kuna msemo kwamba pesa ni sabuni ya roho. Hata hivyo kuna wapenzi ambao hutengana licha ya kuwa na pesa nyingi na mtu kuamua kumwendea asiyekuwa nazo. Je, ni kipi kinachoweza kuchangia hali hii? Wananchi vilevile washauri wa masuala ya ndoa wanatoa kauli zao.
Vijana na Mapenzi Podcast: Mke wa mtu sumu; usimkatie
2021/11/11
Kwa nini baadhi ya wanaume huwachumbia wake za watu wakijua fika kuwa wameolewa? Je, wa kulaumiwa ni nani? Wananchi wanatoa kauli zao kulihusu suala hili vilevile ushauri wa mtaalam.

Podcast reviews

Read Vijana na Mapenzi podcast reviews


0 out of 5
0 reviews

Podcast sponsorship advertising

Start advertising on Vijana na Mapenzi relevant audience podcasts


What do you want to promote?