1578277371
Gumzo na Mwanaspoti

Advertise on podcast: Gumzo na Mwanaspoti

Categories
Country
United States
This podcast has
38 episodes
Language
English
Explicit
No
Date created
2021/07/26
Latest episode
2022/06/19
Average duration
20 min.
Release period
18 days

Description

Ni jukwaa la mazungumzo na wanamichezo kuhusu spoti na maisha yao kwa ujumla. Pia inawahusisha viongozi, wakufunzi na wapenzi wa michezo.

Unlock Gumzo na Mwanaspoti podcast Email contact info,
Listeners & Audience details

Email contact information

Direct podcast contact details

Listeners

Audience numbers & engagement insights

Audience details

Podcast Insights

Podcast episodes

Check latest episodes from Gumzo na Mwanaspoti podcast


Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Magari yetu ni ya viwango vya chini-Dennis Mwenda
2022/06/19
Dennis Mwenda ambaye ni dereva vilevile msaidizi katika mashindano ya Dunia ya Safari Rally anasema magari ambayo yanatumika na Wakenya katika mashindano ya Safari Rally ya WRC ni ya viwango vya chini. Katika mahojiano na mwanahabari wetu, Dennis anasema kutokana na ukosefu wa ufadhili ni vigumu sana kupata magari vya viwango vya juu kutokana na gharama. Dennis ambaye vilevile anaelezea safari yake katika uendeshaji magari ni miongoni mwa madereva ambao watashiriki mashindano ya Safari Rally makala ya mwaka 2022.
Gumzo na Mwanaspoti: Bado tuko kwenye ligi kuu ya FKF - Jakton Obure
2022/06/17
Afisa Mkuu Mtendaji wa Klabu ya Mathare United, Jakton Obure amesema watasalia kwenye ligi kuu ya FKF msimu ujao licha ya kushushwa daraja baada ya kukosa kushiriki mechi tatu mfululizo. Katika mahojiano na Ali Hassan Kauleni na Walter Kinjo, Obure anasema kwa mujibu wa sheria za FIFA ni kwamba kamati ya muda katika shirikisho la soka FKF haina uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu ligi kuu ya soka FKF.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast; Nina tajriba kuwa Rais wa FKF-Allan Wanga
2022/06/03
Allan Wanga anayewania kiti cha urais katika Shirikisho la soka la Kenya [FKF], alikuwa mchezaji wa timu ya Kitaifa ya Soka Harambee Stars. Wanga anaelezea mikakati aliyoweka katika kulenga kuwa Rais wa FKF. Katika mazungumzo na wanahabari wetu Ali Hassan Kauleni na Walter Kinjo, Wanga ambaye ni mfanyakazi katika Kaunti ya Kakamega anasema Kenya inahitajikiongozi ambaye ana ufahamu mkubwa wa masuala ya soka.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Edward Teco, Kupepeta Mpira kumenipandisha ndege
2022/03/20
Edward Teco alianza kupepeta mpira baada ya kupata jeraha uwanjani akiwa shule ya upili hivyo kumlazimisha kuanza Kupepeta mpira ili kuwafurahisha mashabiki wake. Edward ameshiriki mashindano ya Dunia ya Kupepeta Mpira na hata kukutana na baadhi ya mameneja barani Ulaya, akiwamo Pepe Guardiola wa Manchester City. Katika mazungumzo na mwanahabari wetu Walter Kinjo, Edward anaeleza alivyotembea katika mataifa mbalimbali kutokana na taaluma yake ya kupepeta mpira.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Sheryl Aluoch (shabiki wa Gor), nilimwokoa mpenzi wangu
2022/03/05
Shabiki Sugu wa klabu ya Gor Mahia, Sheryl Aluoch kwa mara ya kwanza amezungumzia mvutano ambao ulishuhudiwa kati ya mashabiki wa klabu hiyo na walinzi katika Uwanja wa Kimataifa wa Kasarani mwaka wa.... Aluoch ambaye alionekana kwenye picha na video akiwa amebeba jiwe wakati wa mechi kati ya klabu ya Gor Mahia dhidi ya Vihiga Bullets anasema alilazimika kuingilia kati baada ya mpinziwe kupigwa bila sababu.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Chris Oguso(Police FC) Tunarejesha nidhamu katika Soka. Sehemu 2
2022/02/27
Afisa Mkuu Mtendaji wa Klabu ya Police FC, Chris Oguso anasema watarejesha nidhamu katika soka ya humu nchini. Katika mahojiano na mwanahabari wetu Walter Kinjo pamoja na Rodgers Eshitemi, Oguso anasema nidhamu itaboresha ligi kuu ya FKF vilevile kuwaboresha wachezaji.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Chris Oguso (Polisi FC); maslahi ya wachezaji
2022/02/20
Afisa Mkuu Mtendaji wa Klabu ya Police FC, Chris Oguso anasema wachezaji wengi ambao wanashiriki Ligi Kuu ya FKF wana matumaini ya kujiunga na klabu hiyo kutokana na sheria vilevile maslahi ya wachezaji. Katika mahojiano na wanahabari wetu, Walter Kinjo pamoja na Rodgers Eshitemi, Oguso anasema klabu hiyo imefanya kipaumbele maslahi ya wachezaji ili kuboresha soka na kurejesha imani ya mashabiki kwa Ligi Kuu ya FKF.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Ibrahim Kipkemboi Hussein; ubaguzi wa rangi umepungua Ulaya
2022/01/31
Bingwa mara tatu wa mashindano ya Boston Marathon, Ibrahim Hussein anasema ubaguzi wa rangi umepungua ikilinganishwa na miaka ya awali. Katika mahojiano na Mwanahabari wetu Ali Hassan Kauleni, Hussein ambaye alikuwa Mwafrika wa kwanza kushinda mbio za New York Marathon mwaka 1987 anasema ulikuwapo ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki na hata waandalizi wa mashindano.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Nitawainua wachezaji - Twaha Mbarak, Sehemu ya 2
2022/01/23
Wachezaji katika kaunti zote arubaini na saba nchini watanufaika na uongozi wa Twaha Mbarak iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka FKF. Katika sehemu ya pili ya mahojiano na Ali Hassan Kauleni, Mbarak anasema atawahusisha washikadau wote ili kuhakikisha kwamba wachezaji kutoka kaunti mbalimbali wanajumuishwa katika kikosi cha timu ya kitaifa ya soka Harambee Stars.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast;Kenya kuna Talanta, Twaha Mbarak
2022/01/18
Kwa mara ya kwanza tangu kubuniwa kwa kamati ya muda katika shirikisho la soka Fkf Twaha Mbaruk amezungumzia uongozi wa soka nchini. Katika mahojiano ya mioja kwa moja na Mwanahabari wetu Ali Hassan Kauleni. Twaha amesema Kenya kuna talanta na kwamba ana uwezo wa kuboresha soka hata zaidi.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Moses Kiptanui; Wanariadha wakongwe wametelekezwa. Sehemu 2
2021/12/21
Serikali haiwasaidii wanariadha wakongwe, licha ya kuliwakilisha taifa katika mashindano mbalimbali. Sikiliza podcast hii kuhusu mahojiano kati ya mwanahabari wetu Ali Hassan Kauleni na aliyekuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji, Moses Kiptanui.
Gumzo na Mwanaspoti Podcast: Moses Kiptanui; riadha hadi ufugaji-kwa jeraha
2021/12/13
Aliyekuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji, Moses Kiptanui anasema alipata jeraha hivyo kumlazimu kustaafu mapema. Katika mahojiano ya moja kwa moja na Ali Hassan Kauleni, Kiptanui anasema bado alikuwa na uwezo wa kuwakilisha taifa katika mashindano mbalimbali ya riadha lakini kutokana na jeraha alistaafu mapema.

Podcast reviews

Read Gumzo na Mwanaspoti podcast reviews


0 out of 5
0 reviews

Podcast sponsorship advertising

Start advertising on Gumzo na Mwanaspoti relevant audience podcasts


What do you want to promote?