03 JANUARI 2026
2026/02/03
Hii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa saratani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika hatua ambazo ni uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa kutokomeza saratani ifikapo mwaka 2030.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, leo limetoa ombi la dola bilioni moja ili kukabiliana na majanga ya afya mwaka 2026 katika dharura 36 zilizo mbaya zaidi duniani. Ombi hilo linalenga kusaidia huduma za afya zinazookoa maisha katika nchi zilizoathiriwa na migogoro na majanga, zikiwemo Gaza, Sudan, Haiti na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Mashariki ya Kati, wakati muda ukiendelea kuyoyoma kwa maelfu ya wagonjwa mahututi huko Gaza, kufunguliwa tena kwa kivuko cha Rafah kunaleta mwanga wa matumaini. Kivuko hicho kilifunguliwa Jumatatu baada ya kufungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, chini ya mpango wa amani unaoungwa mkono na Marekani, na kuruhusu uhamisho wa kwanza wa wagonjwa tangu mwaka 2025.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF leo liimesema linaongeza juhudi zake zamsaada wa msimu wa baridi nchini Ukraine huku watoto na familia wakikabiliwa na kukatika kwa umeme, kukosa vipasha joto na maji kufuatia mashambulizi yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya nishati na baridi kali. Tangu Novemba, shirika hilo limesambaza jenereta 106 kote nchini kusaidia huduma za maji na mifumo ya kupasha joto, huku takribani jenereta 150 zaidi zikitarajiwa kuwasili katika wiki zijazo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "KUNVI"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
more