
Advertise on podcast: Kisa Changu
This podcast has
44 episodes
Language
EnglishPublisher
The Standard Group PLCExplicit
No
Date created
2021/07/26
Latest episode
2022/06/25
Average duration
17 min.
Release period
14 days
Description
Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.
Unlock Kisa Changu podcast Email contact info,
Listeners & Audience details
Email contact information
Direct podcast contact details

Listeners
Audience numbers & engagement insights

Audience details
Podcast Insights

Podcast episodes
Check latest episodes from Kisa Changu podcast
Kisa Changu Podcast: Nina hisia tofauti kimwili; si tatizo la kiakili
2022/06/25
Elidah Maita mkazi wa Roysambu, Nairobi ni mwanaharakati wa kutetea haki za watu walio katika uhusiano wa jinsia moja na wa jinsia tambuka yaani ''Queer''.
Anasema alianza kuhisi akiwa tofauti na wasichana wengine akiwa na umri wa miaka kumi pekee na licha ya kumuuliza mamake mzazi maswali chungu nzima hakupata maelezo ambayo yangemsaidia kuelewa hali yake.
Maita mwenye umri wa miaka 25 anasema ari yake ya uanaharakati na kuihamasisha jamii kuhusu ''LGBT-Q+'' ilitokana na changamoto alizopitia alipokuwa mdogo.
Maita anasema watu kama yeye mbali na unyanyapaa wengine wamedhulumiwa bila sababu hali inayowasababishia wengine kukumbwa na msongo wa mawazo huku wengine wakijiua. Mfano anasema mienendo yake na hata jinsi anavyovaa huwafanya baadhi ya watu kumtenga. Hata hivyo, anasisitiza hilo halitazima juhudi zake za kuieleimisha jamii kuhusu LGBT-Q+.
Fahamu mengi zaidi kumhusu Maita katika makala ya ''Kisa Changu Podcast'' na Robert Menza.
Kisa Changu Podcast: Nabaguliwa kwa kuwa nina ulemavu wa ngozi 'albinism'
2022/06/18
Denis Kazungu ni mwenye ulemavu wa ngozi yaani albinism. Kazungu mwenye umri wa miaka 29 na ambaye ni mkazi wa Malindi-Airport, Kilifi anasema hali yake imemsababishia changamoto nyingi tangu alipozaliwa hadi sasa.
Kazungu amepitia unyanyapaa; amebaguliwa si tu na jamii bali pia kwenye maeneo ya kazi akisema ulemavu wake umesababisha kampuni nyingi kutilia shaka uwezo wake wa kutekeleza majukumu.
Je, amefanikiwa vipi na hata kupiga hatua maishani licha ya changamoto hizo? Sikiliza masimulizi yake katika makala yafuatayo ya ''Kisa Changu Podcast'' na Robert Menza.
Kisa Changu Podcast: Mpenzi alinitoroka nilipougua saratani
2022/06/12
Jane Chepchumba mwenye umri wa miaka 32, ni mama wa mtoto mmoja. Chepchumba alianza kuugua saratani ya tumbo mwaka 2012 akiwa katika chuo kikuu.
Anasema alipoanza kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi Mjini Eldoret madaktari walimweleza kwamba huenda asiweze kupata watoto siku za usoni kutokana na athari za saratani. Anasema mpenziwe aliyekuwa naye alivunjwa moyo na hilo na kumwacha.
Anasema baada ya zaidi ya miaka mitano ya matibabu ya Chemotherapy, mwaka 2016 madaktari walimfahamisha kuwa hana saratani tena. Baadaye alifanikiwa kupata mpenzi mwingine ambaye alijaliwa naye mtoto mwaka 2019, ila naye akatoweka. Jepchumba anasema furaha yaka sasa ni mwanawe. Sikiliza masmulizi ya safari ya Jepchumba katika makala haya ya Kisa Changu Podcast.
Kisa Changu Podcast: Kilio cha Mama
2022/04/09
Ruth Keino mkazi wa Nandi ni mama mwenye machungu. Keino amekuwa akitafuta haki tangu mwanawe alipoaga dunia zaidi ya mwaka mmoja uliopita akiwa shuleni.
Beryl Cherop aliyekuwa na miaka 16 alifariki dunia miezi michache tu baada ya kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Upili ya St Teresa of Avila Girls. Kinachomuumiza Keino roho hata zaidi ni kwamba hakuna mtu ahta mmoja aliyehudhuria hafla ya mazishi ya mwanawe kuifariji familia.
Anasema hatachoka hadi pale haki itakapopatikana kufuatia kifo cha mwanawe. Sikiliza masimulizi ya kina katika makala yafuatayo
Kisa Changu Podcast; Jinsi maisha yangu yalivyobadilika baada ya kubandikiziwa figo: Eunice Rop -Sehemu 2
2022/03/20
Baada ya kuhangaika kwa miaka mingi, hatimaye Eunice Rob alifanikiwa kumpata msamaria aliyempa figo kupitia mtandao wa Facebook.
Katika sehemu hii ya pili ya mahojiano na Faith Kutere, Rob anasimulia jinsi maisha yake yamebadilika tangu alipopandikiziwa figo. Pia ana ushauri kuhusu umuhimu wa kufanyiwa ukaguzi wa kiafya mara kwa mara. Sikiliza makala yafuatayo.
Kisa Changu Podcast: Kwa nini niliamua kutumia Facebook kumtafuta mtu anipe figo: Eunice Rop -Sehemu ya Kwanza
2022/03/13
Eunice Rop mkazi wa Nandi Hills alikuwa na matatizo ya kiafya tangu mwaka 2011 ambapo alikuwa akitibiwa katika hospitali moja bila mafanikio.
Mwaka 2013 alitafuta huduma za matibabu katika hospitali moja mjini Eldoret ambapo ilibainika kuwa alikuwa na matatizo ya figo na kuanza matibabu
Mwaka 2015 ndugu zake 2 waljitoleakupata figo nyingine lakini walipofanyika uchunguzi ikagunduliwa wao pia walikuwa na matatizo ya figo.
Baada ya miaka 7 ya matibabu ya figo, mwaka 2019 Mei, Eunice aliamua kutumia mtandao wa Facebook kumtafuta mtu yeyote ambaye angemsaidia kupata figo nyingine.
Je, alifanikiwa? Sikiliza masimulizi ya Eunice na Faith Kutere katika sehemu ya kwanza ya makala yafuatayo.
Kisa Changu Podcast: Waliomuua mume wetu wanatuandamana -Wake wa Isaac Juma
2022/03/06
Zaidi ya miezi miwili tangu aliyekuwa shabiki sugu wa kandanda nchini Isaac Juma kuuliwa, familia yake ya wake wawili na watoto kumi na saba ingali inahangaika. Wakati wa hafla ya mazishi wanawe Juma waliitaka serikali kuwaondoa katika eneo hilo wakidai maisha yao yalikuwa hatarini.
Katika simulizi ifuatayo Wake wa Juma Christine na Farida Juma wamethibitisha madai hayo wakisema watu wasiowajua wamewavamia mara si moja tangu mume wao alipozikwa huku idara za usalama zikisalia kimya.
Mwanahabari Benard Lusigi amewahoji Christine na Farida Juma.
Kisa Changu Podcast: Watoto wa Marehemu Isaac Juma Walilia Haki
2022/02/20
Isaac Juma alikuwa shabiki sugu wa kandanda nchini. Alijijengea jina kwa kuhudhuria na kushabikia Timu ya Kitaifa ya Harambee Stars na ile ya Gor Mahia akiwa amejichora mwili wote kutumia rangi za bendera ya Kenya.
Katika Spoti, Juma alikuwa na wafuasi waliompenda sana wakiwamo mashabiki wenzake. Ila maisha nyumbani kwake yalikuwa tofauti; mbali na kusalia maskini hohehahe licha ya umaarufu huo, ulikuwapo mzozo wa umiliki wa ardhi baina yake na dada zake. Alisema wazi kwamba maisha yake yalikuwa hatarini, huku akiomba ulinzi, lakini alipuuzwa na mwishowe akaangamizwa. Na sasa wanawe wanahofia huenda yaliyompata baba yao yakawapata pia wakitaka kuhamishwa na kupewa eneo mbadala la kuishi.
Aliwaacha watoto 17.14 miongoni mwao wanazungumzia hofu waliyo nayo na mahangaiko marehemu baba yao alipitia kabla ya kifo katika masimulizi haya.
Kisa Changu Podcast: Wanaume wanaochapwa na wake zao wafungua roho
2022/02/06
Visa vya dhuluma za kijinsia vimekuwa zikiripotiwa humu nchini kila kukicha. Hata hivyo mara nyingi utapata kwamba wanawake ndio huwa wepesi wa kuzungumzia dhuluma hizo huku wanaume wakijificha kwa hofu ya unyanyapaa, kuchekwa, kusimangwa na kukejeliwa na wanajamii.
Martin Ndiema amewahoji baadhi ya wanaume wanaopita dhuluma hizo ila wanaogopa kutafuta usaidizi. Sikiliza mahangaiko wanayopitia katika masimulizi yafuatayo.
Kisa Changu Podcast: John Kiriamiti - maisha ya uhalifu; alianzia uandishi jela
2022/02/03
Anafahamika kufuatia visa vyake vya wizi sugu wa pesa katika benki wakati wa miaka ya 70. John Kiriamiti aliacha masomo akiwa katika kidato cha kwanza akiwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Prince of Wales ambayo sasa ni Nairobi School, na hapo ndipo alipoanza uhalifu. Hata hivyo, wasemao husema kwamba siku za mwizi ni arubaini.
Kiriamiti pamoja na wenzake walikamatwa na kuhukumiwa jela kutokana na uhalifu huo. Akiwa jela, John Kiriamiti alianza uandishi wa vitabu, ambavyo baadaye vilikuwa maarufu nchini na kupendwa sana hasa na wanafunzi. Vitabu vilivyoandikwa na Kiriamiti ni kama My Life in Crime, My Life With a Criminal, My Life in Prison. Fahamu zaidi kuhusu maisha yake katika masimulizi yafuatayo.
Kisa Changu Podcast; Kwa nini niliamua kuwasaidia wanaougua fistula - Sharon Korir. Sehemu ya 2
2022/01/30
Katika sehemu ya pili Wakili Korir anaeleza namna mahangaiko yake yalivyompa msukumo wa kuanzisha Shirika la Save a Woman, Fistula Foundation ili kuwapa matumaini wanawake na wasichana ambao wameathiriwa na Fistula.
Akiwa wakili kwa ushirikiano na washikadau mbalimbali, anahisi serikali haijafanya vyema sana katika kuihamasisha jamii kuhusu Fistula hali ambayo imechangia kuwapo kwa unyanyapaa dhidi ya wanawake wanaougua Fistula.
Sikiliza masimulizi haya katika sehemu hii ya pili na Carren Papai.
Kisa changu Podcast; Ugonjwa wa Fistula ulivyoathiri maisha yangu -Sharon Korir Sehemu ya 1
2022/01/23
Wakili Sharon Korir mwathiriwa wa Fistula, anasema alipitia nyingi baada ya kugundua anaugua Fistula ukiwamo unyanyapaa kutoka kwa familia na jamaa zake. Anasema alianza kuugua baada ya kujifungua mwanawe wa pili.
Baada ya kudhalilishwa na hata kutengwa na mumewe alipokuwa na Fistula, Wakili Korir hakukataa tamaa aliamua kumwelezea shemejiye kuhusu tatizo hilo kisha akapata matibabu.
Amezungumza na Carren Papai kuhusu jinsi mambo yalivyoanza, akiwa hospitalini na kipindi cha kupona katika sehemu hii ya kwanza ya Kisa Changu Podcast
Podcast reviews
Read Kisa Changu podcast reviews
Podcast sponsorship advertising
Start advertising on Kisa Changu relevant audience podcasts
You may also like to advertise on these Podcasts

4.8336231
Discover Ag
Tara Vander Dussen & Natalie Kovarik

4.9133412
M&A Science
Kison Patel

4.5170532
Golden State Warriors
Golden State Warriors

4.8189603
Niche Pursuits Podcast: Find Your Next "Niche" Business Idea!
Spencer Haws: NichePursuits.com

4.979460
The Divorce Revolution
Amber Shaw

4.6674421
Marriage Therapy Radio
MTR

4.8251748
Joyful Courage for Parenting Teens
Casey O'Roarty

4.4530149
The Riley Gaines Show
Fox

4.9277238
Moms Overcoming Overwhelm | Decluttering Tips, Declutter, Systems, Routines for Moms, Home Organization
Emily McDermott | I Help Moms Declutter and Get Organized

4.821165
Devils Hockey Network
New Jersey Devils